27 Septemba 2019

27 Septemba 2019

Hii leo Ijumaa ni mada kwa kina ikiangazia taarifa kutoka kwa viongozi wa ujumbe wa Kenya, Burundi na Tanzania kwenye mjadala wa mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA74. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezechiel Nibigira na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi. Katika muhtasari wetu tunamulika faida na hasara za kuwa na fedha kwenye simu, machafuko mapya Nigeria na kuwasili kwa wakimbizi wa Libya nchini Rwanda na neno la wiki ni KAMSA. Karibu na mwenyeji wako ni Grace Kaneiya.

 

Audio Credit:
Grace Kaneiya
Audio Duration:
9'54"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud