Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana mmoja na juhudi zake kunusuru vijana kuepuka vitendo vya kujitoa uhai

Kijana mmoja na juhudi zake kunusuru vijana kuepuka vitendo vya kujitoa uhai

Pakua

Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la afya duniani WHO, inasema kila sekunde 40 mtu mmoja anakufa kwa kujiua. Idadi ya nchi zenye mikakati ya kitaifa ya kuzuia watu kujiua imeongezeka katika kipindi cha miaka mitano tangu shirika hilo lilipotoa ripoti ya kwanza ya dunia kuhusu visa vya kujiua lakini bado idadi ya nchi hizo ni ndogo kwani ni 38 tu duniani kote.

Aidha kwa mujibu wa WHO, kujiua ni sababu ya pili baada ya ajali za barabarani kwa kusababisha vifo miongoni mwa vijana wa umri wa miaka 15 hadi 29.

Katika makala hii, Sheila Akwara ambaye pia ni manusura wa vitendo vya kutaka kujiua sasa akiwa ameanzisha taasisi ya ‘Jenga Africa’ kuwasikiliza na kujaribu kuwanusuru watu na matendo hayo ya kujitoa uhai, ametembelea viunga vya jiji la Nairobi nchini Kenya na kukusanya maoni yanayowasilishwa na Arnold Kayanda.

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Sheila Akwara
Audio Duration
4'6"
Photo Credit
Kwa hisani ya Sheilla Akwara