Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa maji unachangiwa na ukosefu wa miundo mbinu-wakazi Morogoro

Uhaba wa maji unachangiwa na ukosefu wa miundo mbinu-wakazi Morogoro

Pakua

Maji, maji maji! licha ya kwamba maji ni uhai na moja ya mahitaji ya msingi yanahusiana na kila sehemu ya maisha kwa mujibu wa shirika la UMoja wa Mataifalinalohusika na masuala ya maji, UN Water bado watu wengi wanaendelea kukosa huduma hii adhimu kwa sababu mbali mbali ikiwemo; mabadiliko ya tabianchi, majanga na ukosefu wa miundo mbinu. Nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamezungumzia adha ya ukosefu wa maji huku wakistaajabu iweje hawana maji wakati mkoa wao una vyanzo vya maji. Basi ungana na John Kabambala wa radio washirika Tanzania KidsTime FM akimulika hali ya upatikanaji wa maji mkoani humo.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/John Kabambala
Sauti
3'34"
Photo Credit
© UN-Habitat/Kirsten Milhahn