Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kugeuza mafuta ya kupikia kutengeneza dizeli waua ndege wawili kwa jiwe moja

Mradi wa kugeuza mafuta ya kupikia kutengeneza dizeli waua ndege wawili kwa jiwe moja

Pakua

Huku moja wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ikiwa inalenga kutokomeza umaskini,  uvumbuzi ni moja ya muarobaini ambao unategemewa na watu wengi hasa vijana wamejitosa katika mkondo huu wengi wakichochewa sana na ukosefu wa ajira. Sasa wakati akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu, Brian Lukano ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 kutoka Nairobi, Kenya, amegundua kuwa mafuta ya kupikia ambayo yamekwishatumiwa hayatupwi bali yanaweza kusafishwa na kutumiwa tena kwenye magari yanayotumia mafuta aina ya dizeli. Je alifanyaje? Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alizungumza naye kutaka kufahamu zaidi.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi
Audio Duration
3'43"
Photo Credit
MotionECO