Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tusisubiri ajira, tujitolee ili kusaidia jamii zetu- Sharon

Vijana tusisubiri ajira, tujitolee ili kusaidia jamii zetu- Sharon

Pakua

Umoja wa Mataifa hivi sasa umeweka matumaini yake ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa vijana. Chombo kinatambua kuwa mustakabali mzuri wa dunia unawezekana tu iwapo vijana watashiriki wenyewe bila shuruti kuandaa dunia waitakayo na ndio maana Sharon Migariza, wakili kijana kutoka Kenya ameamua kujitolea, kando mwa kazi yake kutatua changamoto kwenye jamii yake, na kujitolea huko kumekuwa na malipo kama anavyosimulia alipohojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Kwanza Sharon anaelezea kile vijana wanakutana nacho mtaani baada ya ndoto zao za kuhitimu shule.

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Stella Vuzo/Sharon Migariza
Audio Duration
3'36"
Photo Credit
UN Photo/Sylvain Liechti