Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya mwanamke  mwenye ulemavu wamulikwa Uganda

Ukatili dhidi ya mwanamke  mwenye ulemavu wamulikwa Uganda

Pakua

Wanawake wenye ulemavu huwa wanakabiliwa na changamoto za kipekee wakilinganishwa na wanaume wenye hali kama hiyo. Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wanawake wenye ulemavu ni pamoja na kufanyiwa ukatili wa kingono, na hatimaye baba wazazi wa watoto wao kuwakana na mara nyingine kufukuzwa na waaume wao pindi, wanawake wanapopata ulemavu wakiwa ndoani.

Changamoto hizo pamoja na unyanyapaa au kubaguliwa katika jamii zinakwamisha safari yao ya kustawi kiuchumi na kijamii. Tuungane na John Kibego anayeleta taswira halisi ya baadhi ya maeneo nchini Uganda katika makala hii akizungumza na Bwana Sula Kasaija, Diwani wa halmashauri ya Manisipaa ya Hoima.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
UNICEF/Sebastian Rich