03 Septemba 2019

3 Septemba 2019

Dorian, kimbunga hiki kilichopiga visiwa vya Bahamas, chasababisha vifo vya watu watano, hali bado si shwari na Umoja wa Mataifa tayari watendaji wake wako nchini humo kusaidia. Tunakwenda DRC ambako shule zimefunguliwa katika maeneo yenye Ebola na UNICEF imechukua hatua kuhakikisha masomo yanaendelea bila hofu, huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kilimo chatumika kuleta amani. Makala leo tunakwenda Uganda kuangazia wanawake wenye ulemavu na ujumuishwaji wao kwenye vikundi na mashinani ni Queen Lisa, mkimbizi aliyeko kambini Kakuma nchini Kenya. Mwenyeji wako leo ni Arnold Kayanda.

Audio Credit:
Arnold Kayanda
Audio Duration:
12'1"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud