Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi kutoka Burundi akiwa kambini Kakuma atumia muziki kubadilisha maisha yake 

Mkimbizi kutoka Burundi akiwa kambini Kakuma atumia muziki kubadilisha maisha yake 

Pakua

Alipoondoka nchini Burundi akiandamana na dada yake mwaka 2009,  msichana Azam Zabimana alikuwa na umri wa miaka 15. Kutokana na taabu na dhiki walizokuwa wanapitia nchini Burundi baada ya kuwapoteza wazazi wao, wasichana hawa walipata msamaria mwema aliyewasafirisha hadi mjini Nairobi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR lilipata kuwahamisha hadi kambi ya Kakuma.Licha ya wao kupitia hali ngumu Azam alijibidiisha na kuwa msanii ambapo hadi sasa amefanikiwa kutunga na kurekodi takriban nyimbo sita. Alizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa Nairobi kuelezea zaidi kuhusu maisha yake. 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
Picha/Siegfried Modola