Je Afrika na Japan uhusiano wao una manufaa yapi? Umoja wa Mataifa umetanabaisha hayo hii leo huko Yokohama ambako kunafanyika mkutano wa 7 wa Tokyo kwa maendeleo ya Afrika, TICADVII. Tunamulika pia majisafi na salama ambapo imebainika kuwa bado mataifa mengi hayawekezi vya kutosha katika maji. Nchini Kenya mradi wa UNHCR wa kuwapatia fedha za ujenzi wakimbizi umeleta nuru. Makala tunammulika kijana mkimbizi kutoka Burundi ambaye sasa anaishi Kenya na anatumia muziki kujikimu maisha yake na ya mwanae. Na mashinani pia tunasalia Kenya. Karibu na mwenyeji wako leo ni Arnold Kayanda.