Utafiti zaidi na maendeleo katika vifaa vya kuzuia malaria na tiba ni muhimu ili kutokomeza malaria katika siku zijazo limesema shirika la afya ulimwenguni, WHO leo Ijumaa kupitia ripoti yake iliyozinduliwa Geneva Uswisi.
Zaidi ya watoto milioni 1.9 wamelazimika kukatisha masomo yao maeneo ya Afrika magharibi na Kati kwa sababu ya ongezeko la mashambulizi na vitisho vya kikatili dhidi ya elimu katika ukanda huo, imesema ripoti mpya ya shrikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyotolewa leo Ijumaa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha utiaji sahihi makubaliano tarehe 21 Agosti 2019 huko Luanda, Angola kati ya marais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda kwa minajili ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Na kwa kina, inaangaziwa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wa Tanzania.