22 Agosti 2019

22 Agosti 2019

Hii leo tunaanza na taarifa kuhusu siku ya kimataifa ya waathirika wa ghasia zitokanazo na dini au imani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anataka wale wote wanaotumia imani au dini kuleta chuki na ghasia wasipewe nafasi. Tutamsikia pia Sarah Tikolo kutoka Kenya, muathirika wa shambulio la kigaidi akisema kile kilichomwezesha kusonga mbele na maisha baada ya kuachwa mjane akiwa na umri wa miaka 21.  Leo pia WHO imesema kuwa chembechembe za plastiki kwenye maji si tatizo kubwa sana kwa binadamu lakini tafiti zaidi zahitajika. Makala tunabisha hodi Morogoro kuangazia adhabu shuleni na mashinani Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tanzania Selemani Jaffo na wito wake kwa vijana. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi

Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
11'52"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud