Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki wangu siyo wa biashara bali ni kuhamasisha jamii yangu katika masula mbalimbali-Kala Jeremiah

Muziki wangu siyo wa biashara bali ni kuhamasisha jamii yangu katika masula mbalimbali-Kala Jeremiah

Pakua

Ziko namna mbalimbali za kushiriki katika utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, yaliyopangwa kuwa yametekelezwa ifikapo mwaka 2030. Kwa upande wa mwanamuziki kijana Kala Jeremiah kutoka Tanzania ambaye pia ni Balozi wa vijana nchini humo, njia ya muziki ndiyo aliyoamua kuitumia kufikisha ujumbe kwa jamii. Muziki wake unatumika katika matamasha mbalimbali yanayolenga kufikisha ujumbe kwa rika mbalimbali, pia akiutumia kupaza sauti za wasio na sauti katika jamii.  Mwamuziki huyu anaeleza kinagaubaga katika mahojiano na Stella Vuzo wa  wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini  Dar es salaa nchini Tanzania.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Kala Jeremiah
Audio Duration
3'41"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania