21 Agosti 2019

21 Agosti 2019

"Nikikutana na magaidi kabla ya kuwasamehe nitawauliza kwanini walitaka kunichinja?" ni kauli ya mmoja wa manusura wa ugaidi nchini Nigeria. Kisha tunamulika vituo vya kulelea watoto Malawi ambavyo vimesaidia kupunguza visa vya ugonjwa wa kipindupindu. Halikadhalika kampuni moja nchini Uholani ambayo imeitikia wito wa kuzalisha vifungashio visivyo vya plastiki. Makala leo ni Kala Jeremiah mwanamuziki kutoka Tanzania na mashinani tunabisha hodi Kenya kwake Winnie Mutevu na ushauri kwa  wale wanaofunga safari kwenda nchi za nje. Mwenyeji wako ni Grace Kaneiya. Karibu!

Audio Credit:
Grace Kaneiya
Audio Duration:
12'27"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud