Uwepo wa wanawake uongozini umeleta matokeo chanya Kenya- Shebesh

20 Agosti 2019

Uwepo wa wanawake katika nafasi za uongozi umezaa matunda na matokeo yake ni dhahiri iwe ni kwa upande wa maswala ya mirathi au hata katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu hususan watoto. Kauli hiyo ni ya Rachel Shebesh, Katibu Tawala kwenye wizara ya maswala ya jinsia, wazee na watoto nchini Kenya ambaye katika mahojiano na Flora Nducha mapema mwaka huu kandoni mwa mkutano kuhusu hali ya wanawake amesema ari ya kisiasa ni muhimu katika kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia.

Bi. Shebesh akizungumzia lengo hilo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema nchi yake imepata faida kutokana na uongozi wa wanawake huku bunge likiwa na wanawake 85 ikilinganishwa na wanawake ishirini hapo awali. Basi sikiliza Makala ifuatayo ambapo Bi.Shebesh anaanza kwa kuelezea baadhi ya tamaduni ambazo ni changamoto ya uongozi miongoni mwa wanawake.

Audio Credit:
Grace Kaneiya/ Flora Nducha/ Rachel Shebesh
Audio Duration:
3'57"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud