Huduma ya kibinadamu ni wito-Wakili Kamunya

19 Agosti 2019

Kutoa huduma ya kibinadamu iwe ni katika mazingira yoyote yale ni wito ambao ni lazima utoke moyoni amesema Ann N. Kamunya wakili mtetezi wa haki za wanawake, raia wa Kenya ambaye sasa yuko Ankara, Uturuki akifanya kazi za huduma za kibinadamu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Ann ambaye hivi karibuni ataenda nchini Botswana kuendelea na huduma hiyohiyo hasa kwa wakimbizi  anasema, suala la kutoa msaada hususan kwa wanawake liko katika damu yake. Na kazi hiyo ya kutetea wasiojiweza kama wanawake, watoto na wakimbizi, iwe kisheria au kwa masuala mengine ya kibinadamu ilikuwa ndoto yake kutokana na mazingira aliyokulia. Ungana na Flora Nducha katika Makala hii ambapo Ann anaanza kumueleza alivyoanza huduma hiyo ya kibinadamu

 

Audio Credit:
Grace Kaneiya /Flora Nducha/ Ann Kamunya
Audio Duration:
6'8"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud