Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 Agosti 2019

19 Agosti 2019

Pakua

Hii leo ni siku ya huduma za kibinadamu duniani na Grace Kaneiya anakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, maudhui ya siku yakiwa ni wanawake wanaotoa huduma za kibinadamu. Tunamulika pia mhudumu wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kisha tunakwenda Uganda ambako mtangazaji wa radio kaanzisha kituo cha kulea watoto yatima, kulikoni? Makala nayo ni Flora Nducha anazungumza na wakili Ann N. Kamunya raia wa Kenya aliyeko nchini Uturuki ambaye anatoa huduma ya kisheria kwa maelfu ya wakimbizi. Anaanza kwa kueleza kilichomchagiza kuwa muhudumu wa masuala ya kibinadamu na mashinani tunakutana na Lucy Gichana kutoka Kenya ambaye ni mwalimu wa kujitolea katika shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum Shanghai, China akizungumuzia umuhimu wa kuzingatia mahitaji na kipawa cha kila mtoto shuleni. Karibu!

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
14'