Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya kunusurika kifo niliamua kuanzisha taasisi ya kusaidia wajane na mayatima-Bi Kamande

Baada ya kunusurika kifo niliamua kuanzisha taasisi ya kusaidia wajane na mayatima-Bi Kamande

Pakua

Dianah Kamande ni mama wa watoto wawili nchini Kenya ambaye katika mazingira ya kushangaza, siku moja mume wake alirejea nyumbani akiwa na nia moja tu, kumuua mkewe, wanaye wawili na kisha yeye mwenyewe ajiue. Ingawa watoto walitoroshwa haraka, mama yao hakuwa na bahati hiyo kwani alikatwakatwa kwa mapanga kichwani na sehemu nyingi za mwili hivi sasa zimepandikizwa vyuma na mishipa ya bandia.

Baada ya tukio hilo Dianah amebakia kuwa mjane kwani mume wake alijiua baada ya kufikiri kuwa ameshamuua mkewe.

Dianah ameanzisha kundi la kuwaleta pamoja wajane ili wasaidiane katika masuala kadha wa kadha.

Flora Nducha alifanya mahojiano na Bi Kamande alipokuwa mjini New York Marekani kuhudhuria kikao cha kimataifa cha hali ya wanawake duniani. 

Audio Credit
Flora Nducha/ Dianah Kamande
Audio Duration
6'22"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman