Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara ya fedha za kigeni mtandaoni yamwinua kijana mmoja nchini Kenya

Biashara ya fedha za kigeni mtandaoni yamwinua kijana mmoja nchini Kenya

Pakua

Akiwa mwanafunzi chuoni nchini Kenya, Paul Mugenda alikuwa na changamoto kubwa za karo hali iliyosababisha  aanze kufanya biashara ndogo ndogo kujikimu chuoni. Hata hivyo siku moja alikutana na mtu aliyemshauri ajaribu biashara ya ununuzi na uuzaji wa fedha za kigeni kwa njia ya kieletroniki ikimaanisha kuwa teknolojia ya mtandao na taarifa za fedha ndio vilikuwa muarobaini kwa shida yake. Kwa muda wa miaka mitano sasa, Paul amekolea katika biashara hii ambayo imeyainua kwa kiwango kikubwa maisha yake kama alivyomweleza mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya  Jason Nyakundi katika makala hii ikiashiria jinsi vijana wanavyoitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kushiriki kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan kutokomeza umaskini na kujikwamua kiuchumi.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ Jason Nyakundi
Audio Duration
4'24"
Photo Credit
AU-UN IST/Stuart Price