Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea
-Dawa mbili zilizoko kwenye majaribio zimeonesha uwezekano mkubwa kutibu Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC lasema shirika la afya duniani, WHO
-Mradi wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat wa kupima ramani za ardhi ni habari njema kwa wakazi vijijini nchini Uganda
-Mradi wa Quid unaoendeshwa na wanawake nchini Italia mbali ya kuhifadhi mazingira umekuwa mkombozi kwa wanawake wanaotoka katika mazingira magumu
-Makala yetu leo inatupeleka Kenya kwa kijana aliyebadili maisha yake kwa kufanya biashara ya kubadili fedha za kigeni mtandaoni
-Na mashinani utamsiki mnadhimu mkuu wa Jeshi nchini Tanzania akizungumzia changamoto za operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa