Mwanamke avunja vikwazo vya kitamaduni kujikimu katika uvuvi, Uganda

13 Agosti 2019

Wanawake huwa ni nguzo muhimu katika mchakato wa maendeleo ya jamii ingawa jambo hili bado halijatambuliwa katika jamii nyingi barani Afrika kutokana na vikwazo vya kitamaduni na fikra potofu. Hata hivyo kuna nuru katika baadhi ya maenneo ambako wanawake wameanza kutoa ushuhuda kuwashawishi wenzao kuchapa kazi zilizozoeleka kufanywa na wanaume kama vile uvuvi na uchuuz ikiwa ni sambamba na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan namba 1 la kutokomeza  umaskini na lile namba 5 la usawa wa jinsia.

Mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda, amemtembelea mmoja wa wanawake wavuvi kwenye ziwa Albert na kuzungumza naye. Mwanamke huyo Leylah Fambe alianza maisha baada ya kutoka shuleni kwa kujishughulisha na biashara ya kuuza vikalmati ambapo alipata fedha za kununua nyavu za kuvua samaki. Sasa ni mmoja wa wavuvi na wachuuzi wa samaki hadi mji mkuu Kampala na miongoni mwa mafanikio ni kusomesha wadogo zake yatima hadi vyuo vikuu kama anavyoeleza katika makala ifuatayo.

(Mahojiano kati ya Kibego na Fambe)

 

Audio Credit:
Grace Kaneiya/John Kibego
Audio Duration:
4'4"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud