13 Agosti 2019

13 Agosti 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, idadi ya watoto walioachwa yatima kutokana na ugonjwa wa Ebola yaongezeka zaidi ya mara mbili sasa msaada wa haraka unahitajika llimesema shirika la UNICEF

-Nchini Mali Umoja wa Mataifa waonya kwamba ukatili dhidi ya watoto na ukiukwaji wa haki zao umefurutu ada

-Wakati maelfu wakiendelea kufungasha virago Venezuela kukimbia machafuko na hali duni ya maisha wakiwa njiani mama mmoja raia wa Ecuador anayemiliki Hosteli awakirimu wakimbizi hao kwa chakula na malazi

-Makala yetu leo iko Uganda utamsikia mwanamke mvuvi na mjasiriliamali akizungumzia mafanikio na changamoto

-Na mashinani tuko Kenya kwa Spika wa Bunge la Seneti Beatrice Elachi

Audio Credit:
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration:
11'17"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud