08 Agosti 2019

8 Agosti 2019

Hii leo Assumpta Massoi anaanzia  na ripoti mpya yenye lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani, watu wanashauriwa kupunguza kula nyama, kulikoni, kisha anakwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ujumbe wa serikali ya taifa hilo na ujumbe kutoka Rwanda wamekuwa na mazungumzo juu ya  kuimarisha uhusiano wao mipakani. Ethiopia nayo imeguswa katika jarida la leo na la msingi zaidi ni hatua za kudhibiti vifo vya wajawazito na watoto, makala ni elimu ya awali na umuhimu wake kwa watoto na mashinani ni Angela Kileo kutoka Tanzania na ushauri wake kwa serikali jinsi ya kuwawezesha vijana, karibu.

Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
11'1"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud