Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa lishe kwa mama na mtoto muhimu katika kufanikisha unyonyeshaji Tanzania

Mradi wa lishe kwa mama na mtoto muhimu katika kufanikisha unyonyeshaji Tanzania

Pakua

Wiki ya unyonyeshaji duniani imefikia kilele chake leo tarehe saba Agosti ambako nchini Tanzania shirika lisilo la kiserikali la CEMDO linalotekeleza mradi wa Lishe Endelevu kwa wilaya sita mkoa wa morogoro kwa ufadhili wa shirika la Save the Children limeelimisha wakazi katika vijiji mbali mbali ikiwemo kijiji cha Lubeho kata ya Lubeho wilaya ya Gairo mkoani Morogoro juu ya unyonyeshaji bora na lishe kwa mama na mtoto. John Kabambala wa radio washirika kids time fm nchini Tanzania alikuwa shuhuda wetu na ametuandalia makala ifauatayo ambapo kwanza kabisa amezungumza na Mariam Mwita, mratibu wa mradi kutoka Save the Children ambaye anaanza kwa kuelezea kuhusu mradi.

 

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kabambala
Audio Duration
3'35"
Photo Credit
UNICEF/Marco Dormino