Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea
-Zimbabwe yaghubikwa na njaa kubwa , Umoja wa Mataifa wasema bila msaada maisha ya mamilioni ya watu yatakuwa hatarini
-Wiki ya unyonyeshaji yafunga pazia , huku shirika la kuhudumia watoto UNICEF Kenya likisema mradi wa lishe wawasaidia kina mama wengi kunyonyesha watoto mazima ya mama pekee
-Huko Mombasa watoto 600 wa kishona waliokuwa hawana utaifa serikali ya Kenya imewapatia vyeti vya kuzaliwa vinavyowasaidia kupata huduma muhimu
-Makala yetu leo inatupeleka Morogoro Tanzania katika wiki ya unyonyeshaji ikimulika lishe
-Mashinani utamsikia binti mkimbizi nchini Panama aliyemwandikia Mungu barua baada ya kubakwa