06 Agosti 2019

6 Agosti 2019

Jaridani hii leo tunaanzia huko Kigali Rwanda na harakati za Umoja wa Mataifa kuhakikisha upatikanaji wa chakula barani Afrika, kisha tunabisha hodi Tanzania kusikia wito wa UNICEF kwa wajiiri ili kuhakikisha wanawake wanapata fursa ya kunyonyesha watoto wao pindi wanapojifungua, baada ya hapo tunakwenda Sudan Kusini kuona jinsi gani Umoja  wa Mataifa unachukua kila hatua kuhakikisha usalama wa raia. Makala yetu inakupeleka Nairobi nchini Kenya kwake mwanamke mmoja mkongwe Cecilia Wangari anayetengeneza redio. Mashinani ni mwanafunzi huko Mbeya Tanzania auzaye ubuyu ili kukidhi mahitaji yake, karibu basi na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
12'48"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud