Fursa ya nishati mbadala yapatikana kutokana  na changamoto ya magugumaji, Uganda.

5 Agosti 2019

Magugumaji ni changamoto inayozikabili mamlaka ya usimamizi wa rasilimali za majini yakiathiri mifumo ya maji na mazingira kwa ujumla ambayo ni msingi wa uhai na maendeleo.  

Nchini Uganda kuenea kwa kasi kwa magugumaji aina ya kariba kumetishia karibu maziwa yote nchini humo kwa karibu muongo mmoja sasa.

Lakini katika utafiti wa mbinu endelevu za kukabiliana na magugu hayo, ushirikiano wa wataalam kutoka serikali ya Misri na serikali ya Uganda umewezesha utekelezaji wa mradi wa majaribio kwenye maziwa ya Kyonga na Albert ambapo magugu haya yanatumika kama nyenzo za kuzalisha gesi ya kupikia kwa mfumo teknolojia ya biogesi.

Pata maelezo zaidi katika makala iliyoandaliwa na mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda baada ya kutembelea wanufaika wa mradi huo kwenye ziwa Albert.

 

Audio Credit:
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration:
3'54"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud