Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Manusura wa Ebola DRC washika hatamu kuepusha kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo

Manusura wa Ebola DRC washika hatamu kuepusha kusambaa zaidi kwa ugonjwa huo

Pakua

Mwaka mmoja baada ya mlipuko wa 10 wa Ebola kwenye jimbo la Kivu Kaskazini  nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, harakati bado zinaendelea kukabiliana na ugonjwa huo ambao  umesababisha vifo vya watu 1800, wawili kati yao ikiwa ni siku chache zilizopita kwenye mji wa Goma. Harakati za kukabili na kudhibiti ugonjwa huo zinahusisha pia manusura ambao wana jukumu kubwa sasa la kusambaza simulizi chanya juu ya uwezekano wa wagonjwa kupona ugonjwa huo hatari na kurejea katika maisha yao ya kawaida kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Sauti
4'1"
Photo Credit
UNICEF/Guy Hubbard