01 Agosti 2019

1 Agosti 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea 

-Wiki ya unyonyeshaji duniani imeanza huku Umoja wa Mataifa ukisisitiza waajiri kuwapa fursa kina mama ikiwemo likizo ya uzazi yenye malipo

-Ikiwa ni miaka 10 tangu kuanza machafuko Kaskazini Mashariki mwa Nigeria hali ya kibinadamu bado ni mbaya na mgogoro unaendelea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP  nchini Tanzania laonesha njia,  kwa kuzindua mfumo wa nishati jua kwenye jengo lake Dar es Salaam

-Makala yetu leo inamulika mwaka mmoja tangu kuzuka kwa mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC

-Na mashinani tunakwenda kwenye kambi  ya wakimbizi wa kipalestina ya Khan Younis huko ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati kuona jinsi kaya inavyohaha kujihudumia katika mazingira duni

Audio Credit:
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration:
12'13"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud