Hii leo jaridani, Grace Kaneiya anaanza na kauli ya mwisho ya Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva ambaye anatamatisha jukumu lake la miaka 10 kwenye shirika hilo akipazia sauti zaidi changamoto ya utipwatipwa. Kisha anaelekea Ulaya ambako wahamiaji walionusurika Mediterania bado wanashikiliwa kwenye boti hadi pale nchi za Ulaya zitakapokubali kuwachukua. Suala pia la huduma za afya Tanzania linamulikwa tukibisha hodi Tanzania kwenye taasisi ya Benjamin Mkapa na makala tupo na SDGs tukiangazia Mulika Tanzania. Mashinani ni jinsi gani mradi wa UNICEF umefungua macho na fikra za wakazi wa Nigeria wawe wanawake au wanaume, Karibu!