Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea
-Kiwanda cha aina yake cha matofali ya plastiki chazinduliwa Cote D'ivoire kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, kuinua kipato na kulinda mazingira kwa msaada wa UNICEF
-Licha ya changamoto na hatari zilizopo mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA una imani kwamba hatua zaweza kupigwa kuelekea amani ya kudumu ya taifa hilo
-Blogu ya Beyond the Lines yawezesha vijana kuelewa lengo la maendeleo yaani SDG #16 linalohusu masuala ya haki na taasisi imara
-Makala yetu leo inatupeleka jijini Nairobi nchini Kenya kuangazia uhifadhi wa mazingira ikiwemo changamoto ya maji taka katika jiji hilo
-Na mashinani utasikia wito na ujumbe wake naibu mkurugenzi wa UN Environment Joyce Msuya katika vita dhidi ya uharibifu wa mazingira