22 Julai 2019

22 Julai 2019

Katika Jarida letu la Habari hii leo Arnold Kayanda anakuletea

-Mkurugenzi mkuu wa shirika la nguvu za atomiki duniani IAEA Yukiya Amano aaga dunia , rambirambi zaendelea kumiminika kutoka kila kona

-Waathirika wa vimbunga Msumbiji wasimulia madhila na kuomba jumuiya ya kimataifa kuwanusuru

-Mshairi kutoka Sudan kusini Bigoa Chuol anahoji kwa wakimbizi nyumbani ni wapi?

-Makala yetu leo inaangazia uchafuzi wa mazingira ya mto Kafu Uganda na athari zake

-Na mashinani tuko Tanzania utasikia wito wa kijana Hussein Melele mratibu na mkurugenzi wa shirika la Mulika Tanzania   linalohusika na kutoa mafunzo kwa jamii kupitia sanaa ikiwemo afya , elimu ya uraia na haki za binadamu.

Audio Credit:
UN News/Arnold Kayanda
Audio Duration:
14'28"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud