Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa maji wa Magik Water waleta majawabu kwa wakabiliwao na uhaba wa maji- Koigi

Mradi wa maji wa Magik Water waleta majawabu kwa wakabiliwao na uhaba wa maji- Koigi

Pakua

Maji ni uhai na bila maji maisha ya mamilioni ya watu yako hatarini kutokana na magonjwa mbalimbali lakini pia kuathiri shughuli zingine zinazotegemea maji ikiwemo uzalishaji wa chakula. Umoja wa Mataifa umekuwa ukitoa wito kwa nchi wanachama kufanya kila mbinu kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa lakini pia kuwa wabunifu ili kuhakikisha rasilimali hii muhimu na adimu iweze kumfikia kila mtu. Kenya ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na changamoto za maji hususan maeneo yanayokabiliwa na ukame na vijijini ambako maji safi ni mtihani kuyapata. Mmoja wa waliopitia changamoto hizo ni Beth Koigi akiwa Chuo Kikuu alifikiria na kuanzisha  mradi wa kipekee kwa jina Majik Water, mradi ambao ni wa kuvuna maji kutoka kwenye hewa, maji ambayo ni safi na salama kunywa. Teknolojia ya mradi huu kwa sasa inatumika nchini Kenya na sehemu mbali mbali za dunia. Huku ubunifu ikiwa moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa, mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alikutana na Bi Koigi na kumuuliza mambo kadhaa kuhusu mradi huu.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Jason Nyakundi
Audio Duration
5'30"
Photo Credit
UN