Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kandanda yawaleta pamoja vijana mahasimu Sudan Kusini

Kandanda yawaleta pamoja vijana mahasimu Sudan Kusini

Pakua

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekamilisha ujenzi wa uwanja wa kandanda nje kidogo ya mji mkuu, Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo. Flora Nducha na taarifa kamili.

Katika uwanja wa mpira wa miguu nje ya mji mkuu wa Sudan Juba, mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sasa imeanza, timu mbili kutoka klabu ya Kor Romla zinachuana katika uwanja huu mpya uliojengwa kwa msaada wa walinda amani wa UNMIS kutoka Thailand na Nepal.

Wasakata gozi waliokumbana na visiki na makorongo uwanjani n ahata kushindwa kufurahia mchezo waupendao inaponyesha mvua sasa wanafuraha na matumaini makubwa akiwemo Uhuru Peter Okimo

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration
1'46"
Photo Credit
UNMISS/ Beatrice Mategwa