Jarida la Habari la Julai 12, 2019

12 Julai 2019

Jaridani leo Julai 12, 2019 na Arnold Kayanda

Leo Habari kwa ufupi kuanzia, ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ANtonio Guterres nchini Msumbiji alikokutana na makundi mbali mbali ya watu na maisha baada ya vimbunga viwili kupiga nchi hiyo.

Mkutano wa nchi zinazochangia vikosi vya ulinzi wa amani, TCCF, umekunja jamvi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjini New York Marekani, mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Luteni Jenerali Yacoub Mohamed azungumza.

Watoto watatu wameuawa katika shambulio dhidi ya shule huko Afrin Kaskazini mwa Syria na kusababisha uharibifu mkubwa wa shule husika limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Mada kwa kina imeangazia utekelezaji wa malengo ya maendeleo nchini Tanzania

Na katika Neno la wiki, linachambuliwa neno KAFALA.

 

Audio Credit:
Arnold Kayanda
Audio Duration:
10'16"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud