Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapitia changamoto nyingi lakini lengo la kuzitimiza SDGs lazima litimie-Emma Bawo

Tunapitia changamoto nyingi lakini lengo la kuzitimiza SDGs lazima litimie-Emma Bawo

Pakua

Imesalia miaka 11 hadi kufikia mwaka 2030 ambao malengo 17 ya maendeleo yanatarajiwa kuwa yametekelezwa kote duniani. Umoja wa mataifa na wadau wake zikiwemo taasisi, serikali, mashirika na watu binafsi wanapambana kuhakisha lengo la utekelezaji linatimbia ingawa safari bado inakumbana na vikwazo.

Shirika la  International Planned Parenthood Federation Africa, IPPFA ni moja ya mashirika yanayosongesha malengo ya maendeleo endelevu kwa kuelimisha jamii hususani wasichana na wanawake kuhusu masuala ya afya ya uzazi nchini Kenya.

Katika mahojiano haya na Grace Kaneiya, Emma Bawo afisa kutoka shirika hilo, anaeleza changamoto wanazoikutana nazo katika harakati zao.

 

Audio Credit
Arnold Kayanda/ Grace Kaneiya
Sauti
3'20"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman