Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuisaidia Afrika kukabili ugaidi asema Antonio Guterres

Jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuisaidia Afrika kukabili ugaidi asema Antonio Guterres

Akizunguma kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Guterres amesema kuwa Afrika inazidi kuwa katika mstari wa mbele katika hatua za kimataifa za kupambana na ugaidi na nchi za Afrika zimefanya jitihada katika kutekelezwa mikakati ya dunia nzima iliyowekwa na Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi.

Bw Guterres ameongeza kuwa kuanzishwa kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi ina maana kuwa kuna mpangalio mzuri kwa kazi ya Umoja wa Mataifa, "tumeipa kipau mbele miradi katika nchi za Afrika kwenye masuala ya kuzuia vitisho kutoka kwa magaidi wa kigeni, kuwapa uwezo na kuwashirikisha vijana, kuzuia ufadhili kwa ugaidi na kuboresha usalama wa safari za hewani. Hivi majuzi niliunda programu ya kusaidia nchi wanachama kuzuia kusafiri kwa magaidi ambayo italenga maeneo ya Upembe ya Afrika na Sahel."

Katibu mkuu ameongeza kuwa angependa kuona ushirikiano mpya wenye nguvu kati ya nchi za Afrika na jamii ya kimataifa katika kupambana na tatizo la ugaidi kwani ugaidi barani Afrika unasambaa na kuitikisa kanda nzima na kwamba  ametiwa wasi wasi na hali ilivyo sasa eneo la Sahel na tisho linalozidi kukua magharibi mwa Afrika, "kuna mifano mizuri ya nchi za Afrika zinashikiana kubadilishana taarifa za kuukabili ugaidi, ujuzi na mbinu bora kama za usalama wa mipakani kuzuia siasa kali kati ya mpaka wa Kenya na Ethiopia kwa msaada wa Umoja wa Mataifa. Ninaamini kuwa mengi yanaweza kufanywa kupanua ushirika huu na mitandaoni na kuliunganisha bara hili dhidi ya vitisho vya ugaidi."

Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenya ambaye aliufungua rasmi mkutano huo amesema Bara la Afrika  limetaabika  sana mikononi na  ugaidi wa kimataifa.

Rais Kenyatta amesema makundi ya kigaidi hususan yale yaliyo washirika wa al Qaeda na mengine, yanahudumu barani Afrika yakichukua himaya, yakivuruga sheria na kuwanyima watu uhuru na hata kuwa tisho kubwa kwa mataifa yanyewe "makundi kama al shabab na Boko haram yameweza kuonyesha kuwa wao ni saratani mbaya inayoanzia sehemu moja au nchi moja na kukua kutoka huko. Kisha makundi haya huwa na athari mbaya sio tu kwa nchi ile lakini pia kwa nchi majirani katika eneo hilo. Wanafanya hivyo sio kwa manufaa ya watu walio chini ya utawala wao dhalimu bali ni njia ya kujitafuta heshima kwa uhalifu wao.

Mkutano huu unawaleta pamoja wajumbe kutoka nchi za Afrika ambao pia watazungumzia suala la athari za ugaidi barani Afrika na suluhu zake, wakiangazia zaidi jinsi nchi zinavyokabiliana na ugaidi huku pia zikiwa zinatatua masuala ya ukosefu wa ajira, mizozo ya kupigania mali asili, umaskini na changamoto za uongozi.

Pakua

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataiafa Antonio Guterres amasema kuwa Jamii ya kimatafa inastahili kuzisaidia nchi za Afrika kupambana na janga la ugaidi. Akiongea mjini Nairobi wakati wa kuanza kwa mkutano wa Afrika dhidi ya ugaidi,  Bw Guterres amesema kuwa dhiki zinazotokana na vitendo vya ugaidi huwaacha waathiriwa na machungu ya muda mrefu.  

Audio Credit
Jason Nyakundi
Audio Duration
3'14"
Photo Credit
UNEP/Duncan Moore