Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika wa kimbunga Idai wawezeshwa na UNFPA Msumbiji

Waathirika wa kimbunga Idai wawezeshwa na UNFPA Msumbiji

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia shirika la Idadi ya watu duniani UNFPA wamekuwa na jukumu kubwa la kuwezesha wanawake mashinani kujikwamua siotu na umasikini bali  katika masuala ya kiafya ikiwa ni pamoja  afya ya uzazi, kupiga vita ukatili wa kijisnia na pia ushauri nasaha kwa waathirika wa magonjwa mbalimbali kama vile VVU na Fistula.

Kwa mujibu wa shirika la UNFPA waathirika wakubwa wa magonjwa hayo ni wanawake  na wengi ni wale wanaoishi katika migogoro ya kivita na maeneo yaliyoathirika na vimbunga kusini mwa bara la Afrika.

Laura Brito ambaye ni mmoja wa manusura wa kimbunga Idai kilichopiga Msumbiji mwaka huu wa 2019, amekuwa mfano wa kuigwa na wengi kwa jitihada zake alizoanzisha kwa msaada ya UNFPA kusaidia wanawake wajawazito  katika mji wa Beira , nchini Msumbiji.

Katika makala hii iliyoandaliwa na Patrick Newman anaeleza kilichopelekea yeye kujitolea kuwasaidia wanawake nchini mwake. Kwa undani zaidi unagana naye katika makala hii.

Audio Duration
4'22"
Photo Credit
UNICEF