Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na harakati za kusaidia wafugaji kukabiliana na ukame Kenya

FAO na harakati za kusaidia wafugaji kukabiliana na ukame Kenya

Pakua

Mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuwa na athari za muda mrefu hususan kwa wafugaji ambao wanategemea maji na malisho kwa mifugo yao. Ukame wa muda mrefu unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi ni moja ya tatizo kubwa kwa wafugaji. Athari zake ni pamoja na kupoteza mifugo, ongezeko la ukosefu wa uhakika wa chakula na ongezeko la umaskini. Nchini Kenya, shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa kutambua changamoto hizo zinazowakabili wafugaji, wamechukua hatua ya kusaidia wakulima hususani nchini Kenya kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji lakini pia malisho kwa ajili ya mifugo wao. Basi kwa undani zaidi ungana na Grace Kaneiya katika mahojiano na Gabriel Rugalema mwakilishi mkazi wa FAO nchini Kenya.

Audio Credit
Patrick Newman/ Grace Kaneiya/ Gabriel Rugalema
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
FAO/Giulio Napolitano