04 Julai 2019

4 Julai 2019

Sikiliza Jarida Maalum la Alhamisi Julai, 4, 2019 leo ikiwa ni siku ya mapumziko hapa Marekani likiangazia -

HABARI KWA UFUPI

-Utafiti wa shirika la kazi ulimwenguni, ILO unaonyesha kwamba ukosefu wa usawa ni wa viwango vya juu katika ulimwengu wa kazi.

-Nchini Jordan, mradi ulioanzishwa na wanawake 6 kwa ajili ya kutengeneza vitamutamu sasa umekuwa na manufaa makubwa siyo tu kwao pekee bali pia kwa jamii zao na ni kutokana na usaidizi kutoka shirika la kazi duniani , ILO.

-Na nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kumefanyika sherehe ya uzinduzi wa jengo la vijana na utamaduni litakalokuwa chini ya wizara ya vijana na maendeleo ya michezo nchini humo kwa lengo la kusongesha amani. Jengo hilo limefadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, MINUSCA.

Na makala ikiangazia ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Audio Credit:
Grace Kaneiya
Audio Duration:
10'47"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud