Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapishi ya Mama Pina aleta nuru kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu Papua New Guinea

Mapishi ya Mama Pina aleta nuru kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu Papua New Guinea

Pakua

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO, ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) mwaka 2016 uliathiri watu  milioni 10.4 huku ukisababisha  vifo vya watu milioni 1.7. WHO inasema kuwa asilimia 90 ya vifo hivyo ni katika nchi maskini na zenye uchumi wa kati.

Umoja wa Mataifa kwa pamoja na washirika wake wamekuwa  wakizihimiza serikali na asasi za kiraia kuwekeza katika miundombinu stahiki ya kiafya ili kutokomeza janga hili ambalo ni  mzigo kwa wakazi wa nchi maskini duniani.

Wito huo umeitikiwa huko nchini Papua New Guinea katika kisiwa cha Daru, ambako mkazi mmoja ajulikanaye kwa jina la Mama Pina ,mpishi na msimamizi katika kituo cha lishe bora amekuwa kivutio na pia msaada kwa wagonjwa wa TB. Je ni kwa vipi? Patrick Newman anafafanua katika makala hii.

Sauti
3'47"
Photo Credit
UN