02 Julai 2019

2 Julai 2019

Hii leo jaridani Grace Kaneiya anaanzia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limelazimika kuongeza operesheni zake za mgao wa chakula kutokana na ghasia zaidi za kikabila. Huko Tanzania harakati za usawa wa jinsia za kuinua wanawake kuangalia zaidi wenye uwezo na si ali mradi tu. Nayo UNESCO yaondoa katika orodha ya maeneo yaliyo hatarini ya urithi wa dunia kanisa ambako yasadikika alizaliwa Yesu huko Bethlehem. Makala ni masuala ya wanawake kutoka Papua New Guinea na mashinani tunabisha hodi Madagascar, mradi wa kukomboa wanawake vijijini. Karibu!

Audio Credit:
Grace Kaneiya
Audio Duration:
10'57"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud