Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilipitia changamoto za wanaume lakini nikawashawishi na kushinda-Mboni Mhita.

Nilipitia changamoto za wanaume lakini nikawashawishi na kushinda-Mboni Mhita.

Pakua

Kwa muda mrefu jamii mbalimbali zimeendelea kukumbatia mfumo dume ambapo wanawake wamekuwa wakipewa nafasi ya nyuma baada ya wanaume, iwe katika elimu, maamuzi katika jamii na hata katika nafasi za uongozi. Ndiyo maana lengo namba 5 la maendeleo endelevu linasisitiza kuhusu usawa wa kijinsia ambapo kila mtu anatakiwa kuwa na haki ya kushiriki katika masuala mbalimbalimbali ya jamii yake bila kujali jinsia yake.

Hata hivyo nchi mbalimbali zimeanza kupiga hatua ya kuleta usawa wa kijinsia ikiwemo Tanzania ambako wanawake wanapewa nafasi ya kushiriki katika ngazi mbalimbali zikiwemo za uwakilishi wa wananchi ijapokuwa bado safari ina vikwazo.

Mboni Mohamed Mhita ni mmoja wa wanawake wachache katika Bunge la Tanzania ambao wamemudu kugombea ubunge kupitia majimbo na hatimaye kupata nafasi ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo la  Handeni, Tanga, kaskazini mwa Tanzania.  Katika mahojiano haya na Arnold Kayanda mjini New York anaanza kwa kueleza moja ya mikutano yake ya hivi karibuni ambayo imeanza kuwahamisha wanawake wengi zaidi kujitokeza katika nafasi mbalimbali.

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
4'13"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman