Njaa Afrika bado ni tishio, azimio la Malabo mashakani

Njaa Afrika bado ni tishio, azimio la Malabo mashakani

Pakua

Licha ya kwamba jitihada kubwa zinafanyika barani Afrika kutokomeza njaa tatizo hilo bado limekita mizizi katika maeneo mengi na hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa haraka ili kuepusha balaa zaidi limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Flora Nducha na taarifa zaidi.

Kandoni mwa mkutano wa 41 wa shirika la FAO unaoendelea mjini Roma Italia, kikao maalumu kimefanyika kikimulika njaa na lishe barani Afrika, dhumuni likiwa ni kutathimini hatua zilizopigwa katika kutekeleza lengo la kutokomeza njaa na utapiamlo katika bara hilo tangu kupitishwa kwa azimio la Malabo 2014 na malengo ya maendeleo endelevu  au SDG’s mwaka 2015. 

Lakini pia kujadili changamoto zilizopo, matarajio, na kubaini hatua za kuchukua, kubadilishana mawazo na uzoefu katika ngazi ya nchi  na kikanda katika kuhakikisha juhudi zinasonga kuelekea kutokomeza njaa ifikapo 2025.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
1'55"
Photo Credit
World Bank/Arne Hoel