Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanafunzi mkimbizi wa DRC atunukiwa tuzo Uganda

Mwanafunzi mkimbizi wa DRC atunukiwa tuzo Uganda

Pakua

Mamilioni ya watu wameendelea kufungasha virago kila uchao kwenda kusaka usalama wakikimbia vita, mateso, mauaji, njaa na sambabu zingine mbalimbali. Japo wakimbizi hawa wanaonekana mzingo machoni mwa wengi Umoja wa Mataifa unasema dunia ikiwakumbatia itaoona mchango wao na faida yao.

Leo ikiwa ni siku ya wakimbizi Umoja huo umetoa wito kwa kila mtu kushikamana na wakimbizi kwani wanachosaka ni amani na kufungasha virago haikuwa kwa hiyari yao. Mfano mzuri wa nchi zinazokumbatia wakimbiz na kuwapa fursa ni Uganda ambayo inahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni moja wengi kutoka Sudan Kusini na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC. Na wakimbizi hao wamedhihirisha kwamba wakishikwa wanashikamana katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu na ajira.

Mfano mzuri ni kijana aliyetunukiwa tuzo kwa kufaulu vyema katika mtihani wa taifa baada ya kupewa fursa ya kusoma. Kwa undani zaidi ungana na mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda katika makala hii.

Audio Duration
4'7"
Photo Credit
© UNHCR/Jordi Matas