20 Juni 2019

20 Juni 2019

Je wajua kuwa vita na mizozo husababisha kiwewe kwa watoto na kuwafanya washindwe kujifunza hata wakiwa ugenini? Ndio maana leo UNESCO inataka walimu wapatiwe mafunzo ili wahimili changamoto za kufundisha watoto wakimbizi wenye kiwewe. Hii ni moja ya habari zetu leo siku ya wakimbizi duniani. Tunamulika pia harakati za FAO za kuepusha mizozo kati ya wenyeji na wakimbizi wakati huu Katibu Mkuu anataka mshikamano na wakimbizi. Tunaangazia pia ugonjwa wa kifafa na unyanyapaa wanaopata wagonjwa ambapo wengine hukatazwa hata kuoa au kuolewa. Makala ni mkimbizi aliyeibuka kidedea huko Uganda na mashinani madhila wanayopata wanawake na wasichana kwenye mzozo unaoendelea huko DR Congo. Karibu na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
11'48"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud