19 Juni 2019

19 Juni 2019

Leo ni siku ya kimataifa ya kukabiliana na ukatili wa kingono kwenye maeneo ya mizozo na tunamulika kauli ya Umoja wa Mataifa inayosema kuwa ukatili huo ni msalaba kwa wote na hivyo hatua zichukuliwe kusaidia manusura. Kuelekea kesho siku ya wakimbizi tunajulishwa kuwa idadi ya wakimbizi imevuka milioni 70 na sasa kinachotakiwa siyo tu kukomesha mizozo bali pia kuonyesha mshikamano na wale waliofurushwa. Tunakutana na kijana Mustafa, mkimbizi kutoka Somalia akisema kuwa, "mkisikia simulizi zetu basi hamtotuchukia." Makala leo ni kijana Isaya Yunge kutoka Tanzania, ingawa sasa maisha yanaonekana kumnyookea lakini safari yake ilikuwa na shubiri lakini hakukata tamaa. Mashinani ni manusura wa kingono akipaza sauti. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit:
Flora Nducha
Audio Duration:
12'57"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud