Miradi ya MONUSCO ni neema kwetu:Waathirika wa ukatili wa kingono

18 Juni 2019

Ukatili wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia ni moja ya changamoto kubwa katika maeneo yenye vita na waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana. Manusura hawa hujikuta hawana msaada wala pa kushika baada ya wengine kuachwa na ujauzito , watoto na hata maradhi. Mathalani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa kushirikiana na mfuko maalum wa msaada kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono TF wanawasaidia wanawake waathirika na watoto wao waliozaliwa kupitia unyanyasaji huo uliofanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Ungana na Patrick Newman kwa makala hii.

Audio Credit:
Assumpta Massoi/Patrick Newman
Audio Duration:
3'47"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud