Ingawa kuna changamoto angalau Kenya imechukua hatua kutulinda watu wenye ulemavu wa ngozi- Mbunge Mwaura

13 Juni 2019

Tarehe 13 mwezi Juni ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha jamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu wa ngozi. Siku hii inaadhimishwa kwa kuzingatia changamoto wanazokabiliana nazo kundi hilo ikiwemo kutengwa, kunyanyapaliwa na pia hata kuuawa kwa fikra potofu ya kwamba viungo vyao vinaweza kutumika kwa ajili ya utajiri.

Nchini Kenya, moja ya mataifa ambayo kundi hilo limekumbwa na changamoto, tayari kuna watetezi ndani ya kundi hilo na miongoni mwao ni Isaac Mwaura, mlemavu wa ngozi ambaye ni wa kwanza kuchaguliwa kuwa mbunge kwenye bunge la Kenya.

Bwana Mwaura katika mahojiaono na mwandishi wetu Jason Nyakundi huko Nairobi, Kenya anaanza kwa kuelezea changamoto wanazokumbana nazo.

Audio Duration:
3'31"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud