Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiwa na ulemavu wa Ngozi hata kupata mwenza ni mtihani:Chinemba

Ukiwa na ulemavu wa Ngozi hata kupata mwenza ni mtihani:Chinemba

Pakua

Changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa Ngozi ni nyingi, kuanzia unyanyapaa, kuporwa haki zao za kuishi, kupata elimu, kuthaminiwa na hata kupata wenza katika maisha. Changamoto hizi zimeufanya Umoja wa Mataifa kulivalia njua suala la kuhamasisha jamii kwa kuzielimisha kuwa watu wenye ulemavu wa Ngozi ni sawa na watu wengine na wanastahili haki kama wengine. Umezitaka nchi wanachama kuchukua hatua madhubuti ikiwemo sheria ili kuwalinda watu hawa na haki zao. Tanzania ambako kwa muda umekuwa ni mtihani mkubwa kuishi na ulemavu wa Ngozi sasa juhudi kubwa zinafanyika kuanzia ngazi ya jamii kuhakikisha watu hao na haki zao zinalindwa. Katika kuelekea siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu watu wenye ulemavu wa Ngozi hapo Juni 13, iliyobeba kaulimbiu “afya bora na ustawi kwa wote”  John Kabambala amezungumza na kisjana Janeth Chinemba mwanaharakati na balozi wa watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani Morogoro nchini humo na amemweleza kwa nini amelivalia njuga suala la kupigania haki za watu hawa inga yeye mwenye hana ulemavu wa Ngozi.

Audio Credit
Arnold Kayanda
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UNICEF/Frank Dejongh