Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taka za plastiki sio tu uchafu bali ni gharama- January Makamba

Taka za plastiki sio tu uchafu bali ni gharama- January Makamba

Pakua

Changamoto za taka za plastiki sio tu katika uchafuzi wa mazingira na athari kwa afya za binadamu, bali pia ni gharama kubwa kuzikusanya na kuzitokomeza ikiwemo mifuko ya plastilki. Umoja wa Mataifa unasema ili kufanikisha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs hasa katika kulinda na kuhifadhi mazingira taka za plastiki ni lazima zikomeshwe. Tanzania miongoni mwa nchi wanachama zinazochukua hatua za kutimiza wito huo na imeanza kutekeleza rasmi sheria ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki mwishoni mwa wiki Juni Mosi . Katika makala hii Flora Nducha anazungumza na Waziri wa Mazingira wa nchi hiyo January Makamba ambaye amemweleza kuwa miaka kadhaa iliyopita mifuko ya plastiki haikuwepo na sasa ni wakati wa kurejea zama hizo.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration
4'16"
Photo Credit
Saeed Rashid